Партнерка на США и Канаду по недвижимости, выплаты в крипто

  • 30% recurring commission
  • Выплаты в USDT
  • Вывод каждую неделю
  • Комиссия до 5 лет за каждого referral

NAFASI ZA KAZI YA KUJITOLEA:

MWEZESHAJI WA VIKUNDI VYA WANAWAKE VIJANA

(Waombaji Nafasi hizi za kazi ni lazima binti ama mwanamke kijana tu)

NAFASI ZA KAZI YA KUJITOLEA: Mwezeshaji wa Vikundi vya Wanawake Vijana

KITUO CHA KAZI: Itakuwa ndani ya kata husika za mradi

MUDA : Mwaka mmoja

PASADA kupitia Sauti za Watanzania ni mradi wa miaka mitano wa USAID na PEPFAR unaotekelezwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili kuyafikishia makundi maalum na yale yaliyo katika mazingira hatarishi na huduma  bora za kujikinga na maambukizi ya VVU pamoja na uzazi wa mpango katika mikoa mitano iliyopewa kipaumbele nchini Tanzania. Mradi unasimamiwa na Shirika la Jhpiego na washirika wake kwa kupitia Asasi za kiraia katika mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya Shinyanga na Dar es Salaam.

Mwezeshaji wa vikundi vya Mabinti na wanawake vijana ni binti au mwanamke kijana ambaye atakuwa mstari wa mbele katika kuwahamasisha mabinti na wanawake vijana ambao wako kwenye hatari ya kupata maambukizi ya VVU. Kuwawezesha ili wakue kiuchumi, kijamii kupitia vikundi vya WORTH chini ya mradi wa Sauti. Walengwa wa mpango huu watajiunga katika vikundi ambako watajifunza namna ya kuunda na kuendesha vikundi vya kujiwekea akiba na kukopa, elimu ya fedha, namna ya kujikinga na maambukizi ya VVU, njia za uzazi wa mpango, Ukatili wa kijinsia, Malezi chanya ya watoto, mawasiliano ya kubadili tabia na huduma ya afya ya uzazi. Pia walengwa wataunganishwa na huduma rafiki za afya ya uzazi, kupima VVU na huduma endelevu.

НЕ нашли? Не то? Что вы ищете?

MAELEZO KUHUSU MAJUKUMU YA MWEZESHAJI WA VIKUNDI.

1.  Kusuaidia kuendesha mafunzo kwa wanavikundi ili waweze kujua kusoma na kuandika,

2.  Kusaidia kuunda benki za kijiji (Vikundi vya WORTH) zilizo imara pamoja na kuanzisha na kuendesha biashara zinazoleta faida kwa walengwa

3.  Kusaidia kuwafundisha Viongozi wa vikundindi ili waweze kuwa viongozi wazuri na imara na kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ya uongozi kwa ufanisi mkubwa, haki na uwazi.

4.  Kuhakiksha kuwa vifaa-kazi vinavyotolewa na mpango vinagawanywa vizuri na pia kuweka kumbukumbu za kugawanywa kwa vifaa hivyo au vijitabu vingine vya kujifunzia.

5.  Kuendesha vipengele 8 vya mafunzo juu ya malezi na matunzo bora ya watoto.

6.  Kuendesha vipengela 13 vya namna ya kuendesha kikundi, kutunza mikopo, akiba na uongozi wa vikundi.

7.  Kuendesha vipengele 10 vya mafunzo juu ya mawasilino ya kubadili tabia.

8.  Kuandaa na kuwasilisha ripoti za kutembelea vikundi za kila wiki pamoja na ripoti ya kila mwezi kuhusu shughuli zake.

9.  Kushirikiana kwa karibu na Waelimisha rika kuhamasisha na kuwatambua walengwa.

10.  Kuwashauri na kuwaunganisha walengwa na huduma za kupima, huduma ya afya uzazi, huduma kwa ukatili wa kijinsi nk.

SIFA NA UZOEFU UNAOTAKIWA:

1.  Awe Msichana (asiyepungua umri wa miaka 18 na asiyezidi miaka 30)

2.  Awe amemaliza kidato cha nne na mafunzo ya mwaka mmoja kwenye mambo ya kijamii

3.  Cheti cha mafunzo ya maendeleo ya jamii kitakuwa sifa ya ziada

4.  Awe na uzoefu wa angalao miaka mitatu ya kufanya kazi na wasichana au wanawake vijana katika ngazi za chini katika jamii

5.  Awe na uwezo mzuri wa mawasiliano ya kuandika na kuzungumza katika lugha ya jamii husika pamoja na lugha ya taifa.

6.  Awe ana uwezo wa kuandika ripoti ya kazi kwa juma au mwezi.

7.  Awe na uwezo mzuri wa kufundisha, na uwezo wa kuhamasisha jamii

8.  Awe na uwezo na utayari wa kufanya kazi katika muda tofauti itakavyohitajika na pia awe binti au mwanamke kijana ambaye hatahitaji usimamizi wa karibu wa mtu mwingine

9.  Aweze kufanya kazi na wadau wengine wa mpango huu ili kuhakikisha kuwa walengwa wanapata huduma stahiki na rafiki

10.  Awe na sifa ya kuheshimu wengine na kutokuwa mbaguzi kwa namna yeyote.

11.  Awe anajua kuendesha baiskeli na tayari kuitumia kwa kazi

Mtu yeyote ambaye anazo sifa zilizotajwa hapo juu awe huru kuandika barua yake ya kuomba kazi hii ya kujitolea na awasilishe barua ya maombi yake ya kazi na muhtasari wa habari zake binafsi (CV) pamoja na nakala za vyeti. Maombi hayo yapitie kwa mtendaji wa Kata na barua zitumwe kwa;

Mkurugenzi Mtendaji

PASADA,

S. L.P 70225

Dar es salaam

Barua zote ziwasilishwe kwa mkono kwenye ofisi za PaSADA zilizopo Chang’ombe Ndani ya Kanisa Ktoliki ofisi imetazamana na Polisi Mkoa wa Temeke Chang’ombe kabla ya tarehe 3/3/2016.

Kata zitakazohusika na mradi huu ni:

1. Kigamboni

2. Vijibweni

3. Kisarawe II

4. Somangila

5. Toangoma

6. Keko

7. Kurasini

8. Pemba mnazi

9. Mjimwema